Wednesday, October 3, 2007

World Teachers Day:How do you find it?


Hallow Mwalimu,
Pole na majukumu yako ya kila siku.Kwa muda mrefu nimekuwa kimya pasipo kukuandikia kutokana na ndoa yangu na Kaisari kutoashiria kuwa na mashaka jambo linalonifanya nijibidiishe sana katika kazi ili niweze kumshawishi asinipe talaka.

Leo nimeamua kutumia muda huu mdogo wa chai kukuandikia japo kidogo.Siku ya mwalimu Duniani ndiyo iliyonipa morali wa kukuandikia Mwalimu.

Tarehe 5 Oktoba ya kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya Mwalimu.Siku hii kwa hapa kwetu Tanzania huratibiwa na kudhibitiwa na Chama cha walimu Tanzania(CWT) .Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana maadhimisho hayo kila mwaka tangu nilipotambua kuwa kuna kitu kama siku ya mwalimu.Hivi mwalimu unatambua kweli kiini cha siku hii ya mwalimu na madhumuni yake?

Katika maadhimisho yote niliyopata kuhudhuria katika mikoa ya kanda ya mashariki kikubwa kinachofanyika katika maadhimisho hayo huwa ni maandamano, mashindano ya kufukuza kuku,kutembea ukiwa ndani ya gunia,mashindano ya kula,ngoma za kuhamasishana ,kwaya,riadha na mashindano mengine yanayoonekana kufaa kwa wahusika.Mwisho wa yote huwa ni-kujimuvuzisha kwenda mahali fulani kwa wahusika fulani kwa ajili ya "kukata mti na kupanda mti" vijana wa kijiweni wanaita "Kujiachia"

Mwalimu,hapo juu nimekuuliza hivi kweli tunajua kiini cha kuanzishwa kwa siku hiyo na madhumuni yake?Mimi sijui ila bado najaribu kutafuta ukweli katika hilo.Inawezekana waratibu wake hapa nchini(CWT) wanajua.Katika ujumbe wangu huu kwako leo sitaki kabisa kugusia kuhusu CWT na Mustakabali wa taaluma ya Ualimu na Elimu Tanzania kwani ni mada nitakayoizungumzia siku nyingine kipekee.Ila ombi langu kwako ni mabadiliko ya "kimtazamo kuhusu siku ya mwalimu."

Mwalimu! nazungumzia kubadili mtazamo kutoka katika kuadhimisha kwa kufanya mambo tuliyoyazoea na kuangalia namna tunavyoweza kufanya-Professionalization of Teaching profession kwa kutumia siku hii ya mwalimu.Hili linawezekana ikiwa tu walimu wataandaliwa na kupewa nafasi ya kuandika papers na kuziwasilisha katika maadhimisho hayo katika ngazi zote.Yaani kuanzia katika vituo vyao vya kazi hadi kitaifa.Teana ikiwezekana hapa kwetu tuwe na wiki ya mwalimu badala ya siku ya mwalimu.Kwa mwaka huu unaweza kuwa umechelewa kwa kuwa zimebaki siku tatu tu kama sijakosea.Lakini ni matumaini yangu kuwa hii ni nafasi yako kujadili na mwalimu mwenzako na kufikisha ujumbe huu kwa walimu wengine na kuona ni kwa namna gani tunaweza kuifanya siku hii ya mwalimu kuwa ni yenye manufaa zaidi kwa taaluma ya Ualimu na maendeleo ya Elimu nchini.

Mwenzenu,

____________ _________ _________ _________ _________ _________ _
Without "Ethical Culture" there is No Salvation for Humanity
____________ _________ _________ _________ _______

No comments: