Wednesday, October 3, 2007

Kimepotelea Wapi kizazi hiki?

Poleni kwa mihangaiko ya hapa na pale.Nimeona si vibaya nikashiriki pamoja nanyi katika kujiuliza maswali ambayo japo sio mara yangu ya kwanza kujiuliza but yaliibuka kwa kasi jana nilipoamua kuingia mtaani pasipo dhamira yoyote baada ya kupata taarifa ya kuahirishwa kwa kikao cha kamati ndogo ya "Infomal network of young Tanzanian Intellectuals (wanazuoni) pale Mzalendo Pub-Kijitonyama.

Kimepotelea wapi kizazi hiki? ni swali nililobaki kujiuliza hata sasa kutokana na yaliyojili katika mazungumzo na watu mbalimbali katika matembezi yangu.

1. Kimepotelea wapi kizazi hiki?

* Kizazi cha vijana wa kitanzania waliokuwa tayari kupingana na itikeli za maisha zilizowalazimisha kuyakubali yale wasiyoyaafiki kuwa ndio msingi wa ujenzi wa jamii wanayoitaka?

* Kimepotelea wapi kizazi cha vijana wazalendo waliokuwa tayari kuifia nchi yao kwa kuipigania kwa kwa lolote waliloamini ni kinyume na matarajio ya jamii yao?

* Wapo wapi wanawake ambao walikuwa tayari kusema hapana kwa mali na ndio kwa mapenzi ya dhati katika hali iwayo yote ile waliyonayo hao wawapendao?

* Kimepotelea wapi kizazi cha wanawake wenye huruma ambao hawakuwa tayari kuharibu mimba ya watoto waliowabeba?

* Kizazi cha wanawake waliokuwa tayari kubeba mimba miezi tisa na kulea watoto wao?

* Wanawake waliokuwa tayari kulea watoto wa wengine?

* Kizazi cha wanawake waliokuwa tayari kuanza maisha ya pamoja na wenzi wao/waume zao/wao wakiwa hawajui waanze vipi?wakiwa hawana hiki wa kile,waliokuwa tayari kuwasubiri wenzi wao kuwa muda wowote wawapo mbali na upeo wa macho yao?

* Kimepotelea wapi kizazi cha kile ambacho wazazi na walezi waliokuwa tayari kuwaonya watoto wa wengine waliowaona wakipotoka popote walipowaona?

* Kikowapi kizazi cha watoto wale waliokuwa taayari kuacha michezo yao na kuwasaidia wazee wasiojiweza na wote waliowazidi umri mizigo yao hadi wakotaka kufika na kurudi kuendelea na michezo yao?

2. Wazazi kwanini mmeacha kuzaa kizazi hicho?au
mmekwenda likizo ya uzazi
hadi hapo mtakapobaini kiu ya uhitaji wa Dunia kuwa
na watu wa aina hiyo?

3. Je,ni wakati gani huo mnao usubiri kama sio sasa?

4. Wakunga kwanini mmeacha kuzalisha watu aina hiyo
ilihali Tanzania,Africa na Dunia inawahitaji?


* Je,hali hii itaachwa hadi lini?
* Intellectuals wanafanya nini kuinusuru jamii kutoka katika ghalika(Angamizo kuu)

Aaah!Dhambi hii tutaungama wapi?

Mwenzenu,
Malata

No comments: