Friday, October 19, 2007

Teaching Occupation in Tanzania in relation to Professionalism


Leo tena nimeamua kukuandikia ujumbe mwalimu wa Tanzania.Hata hivyo mjadala huu unaweza pia kujadiliwa nasi wote katika jumuia yetu. Mwalimu, nasikia eti zile kauli "zilizopendwa" za ualimu ni wito zinaendelea kupeperushwa hewani.Uzushi huo na wanaodai hivyo usiwasikilize hao!!!!!! Mwalimu,Mobile phone ndiyo iliyonifanya nipate msukumo wa kukuandikia ujumbe huu.Hapo juu nimekuasa usiwasikilize wanaodai kuwa "ualimu ni wito" kwa sababu zifuatazo.Juzi nilipokuwa narudi nyumbani nikiwa katika usafiri wa jumuia kaka mmoja alikuwa akiongea kwenye simu yake ya kiganjani.Sehemu ya maongezi yake alisema hivi,Nanukuu;
.."Yaani wewe hata ualimu tu umekosa?Kwani
ulipata pointi ngapi? eti!! pointi 30?Acha kuzubaa wewe nenda kasomee ualimu!!..
.."


M
walimu! eti ualimu ni wito! nani kasema?kwangu ualimu ni kazi kama kazi kazi nyingine.Labda sasa naanza kufikiri kauli mbadala kuhusu Ualimu.Inawezekana ualimu ni taaluma ya watu walioshindwa maisha!!!?yaani watu waliokosa mwelekeo wa maisha .Kama hivyo sivyo,ni kitu gani kinapelekea watu kufikia hatua ya kusema ".......hata ualimu tu umekosa......"?

Mwalimu! sitaki kuisadikisha nafssi yangu kuwa wewe ni mchovu na umeingia kwenye taaluma ya Ualimu kwa kuwa hukuwa na uchaguzi mwingine wa kufanya maisha mtaani.Kama hivyo ndivyo kwako,Tafadhali usipoteze muda wako bure,AMKA FUNGASHA UENDE!!!!
Nasema tena na tena wajamane! Ualimu ni taaluma kama taaluma nyingine.Ukijaribu kujimuvuzisha katika Oxford Advanced Learners Dictionary(1998) a profession is defined as a paid occupation,especially one that requires advanced education and training.Na kama ulikuwa haujui,ualimu ni taaluma pia yenye sifa na vigezo karibu vyote vya kazi ya kitaalamu kama Carr & Kemmis(1986) wanavyojaribu kubainisha sifa za kipekee za taaluma.Wanasema;Nanukuu.
"........First of all,a profession consist of members whose methods and procedures of working are based on a body of theoretical knowledge and research. Secondly,a professions have ethical codes which govern their members to ensure that they work with commitment towards the well-being of their clients. Thirdly,in order to make sure that they always work to serve the interest of their clients,professions reserve the right to autonomous judgment free from external non-professional control and constraints..."

Ijapokuwa kuna vigezo vingine vingi vinavyopaswa kuzingatiwa katika kuainisha kazi za kitaaluma,bado nasisitiza kuwa Ualimu ni taaluma kama taaluma nyingine .


Samahani mwalimu nisije nikakuchosha ukashindwa kufanya lesson preparation.Hata hivyo naomba unipe dakika chache ili nimalizie ujumbe wangu.Mwalimu! mimi kwa haraka haraka na kwa akili zangu kidogo nimejifunza kitu fulani ambacho walimu tunapungukiwa nacho.Walimu wa Tanzania hatuna chama cha kitaaluma.(Professional Body).What we have is just a trade union(CWT) which have got nothing to do with professionalization of the teaching profession.
Mwalimu ,katika kufikiri nini cha kufanya ili kuipa hadhi taaaluma ya ualimu hapa nchini tujifunze from other professional bodies like that of engineers,medical doctors or NBAA.Kwa kufanya hivyo labda tutaweza kuwazuia watu wasio na taaluma ya ualimu kuthubutu kufanya maamuzi mazito kuhusu mabadiliko ya mitaala ya elimu nchini kama tulivyopata kushuhudia siku za karibuni.

Mwalimu,am very sorry as I am getting confused as I don't know what am I writing.But what I know for sure is that I am writing to mwalimu wa Tanzania.As long as you have the lesson plan,lesson notes and the teaching aids,Please get ready for lesson presentation and lets meet again next time on the discussion about "CWT na Mustakabali wa Elimu na Ualimu Tanzani"

Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania.

Mwenzenu


Wednesday, October 3, 2007

Kimepotelea Wapi kizazi hiki?

Poleni kwa mihangaiko ya hapa na pale.Nimeona si vibaya nikashiriki pamoja nanyi katika kujiuliza maswali ambayo japo sio mara yangu ya kwanza kujiuliza but yaliibuka kwa kasi jana nilipoamua kuingia mtaani pasipo dhamira yoyote baada ya kupata taarifa ya kuahirishwa kwa kikao cha kamati ndogo ya "Infomal network of young Tanzanian Intellectuals (wanazuoni) pale Mzalendo Pub-Kijitonyama.

Kimepotelea wapi kizazi hiki? ni swali nililobaki kujiuliza hata sasa kutokana na yaliyojili katika mazungumzo na watu mbalimbali katika matembezi yangu.

1. Kimepotelea wapi kizazi hiki?

* Kizazi cha vijana wa kitanzania waliokuwa tayari kupingana na itikeli za maisha zilizowalazimisha kuyakubali yale wasiyoyaafiki kuwa ndio msingi wa ujenzi wa jamii wanayoitaka?

* Kimepotelea wapi kizazi cha vijana wazalendo waliokuwa tayari kuifia nchi yao kwa kuipigania kwa kwa lolote waliloamini ni kinyume na matarajio ya jamii yao?

* Wapo wapi wanawake ambao walikuwa tayari kusema hapana kwa mali na ndio kwa mapenzi ya dhati katika hali iwayo yote ile waliyonayo hao wawapendao?

* Kimepotelea wapi kizazi cha wanawake wenye huruma ambao hawakuwa tayari kuharibu mimba ya watoto waliowabeba?

* Kizazi cha wanawake waliokuwa tayari kubeba mimba miezi tisa na kulea watoto wao?

* Wanawake waliokuwa tayari kulea watoto wa wengine?

* Kizazi cha wanawake waliokuwa tayari kuanza maisha ya pamoja na wenzi wao/waume zao/wao wakiwa hawajui waanze vipi?wakiwa hawana hiki wa kile,waliokuwa tayari kuwasubiri wenzi wao kuwa muda wowote wawapo mbali na upeo wa macho yao?

* Kimepotelea wapi kizazi cha kile ambacho wazazi na walezi waliokuwa tayari kuwaonya watoto wa wengine waliowaona wakipotoka popote walipowaona?

* Kikowapi kizazi cha watoto wale waliokuwa taayari kuacha michezo yao na kuwasaidia wazee wasiojiweza na wote waliowazidi umri mizigo yao hadi wakotaka kufika na kurudi kuendelea na michezo yao?

2. Wazazi kwanini mmeacha kuzaa kizazi hicho?au
mmekwenda likizo ya uzazi
hadi hapo mtakapobaini kiu ya uhitaji wa Dunia kuwa
na watu wa aina hiyo?

3. Je,ni wakati gani huo mnao usubiri kama sio sasa?

4. Wakunga kwanini mmeacha kuzalisha watu aina hiyo
ilihali Tanzania,Africa na Dunia inawahitaji?


* Je,hali hii itaachwa hadi lini?
* Intellectuals wanafanya nini kuinusuru jamii kutoka katika ghalika(Angamizo kuu)

Aaah!Dhambi hii tutaungama wapi?

Mwenzenu,
Malata

World Teachers Day:How do you find it?


Hallow Mwalimu,
Pole na majukumu yako ya kila siku.Kwa muda mrefu nimekuwa kimya pasipo kukuandikia kutokana na ndoa yangu na Kaisari kutoashiria kuwa na mashaka jambo linalonifanya nijibidiishe sana katika kazi ili niweze kumshawishi asinipe talaka.

Leo nimeamua kutumia muda huu mdogo wa chai kukuandikia japo kidogo.Siku ya mwalimu Duniani ndiyo iliyonipa morali wa kukuandikia Mwalimu.

Tarehe 5 Oktoba ya kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya Mwalimu.Siku hii kwa hapa kwetu Tanzania huratibiwa na kudhibitiwa na Chama cha walimu Tanzania(CWT) .Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana maadhimisho hayo kila mwaka tangu nilipotambua kuwa kuna kitu kama siku ya mwalimu.Hivi mwalimu unatambua kweli kiini cha siku hii ya mwalimu na madhumuni yake?

Katika maadhimisho yote niliyopata kuhudhuria katika mikoa ya kanda ya mashariki kikubwa kinachofanyika katika maadhimisho hayo huwa ni maandamano, mashindano ya kufukuza kuku,kutembea ukiwa ndani ya gunia,mashindano ya kula,ngoma za kuhamasishana ,kwaya,riadha na mashindano mengine yanayoonekana kufaa kwa wahusika.Mwisho wa yote huwa ni-kujimuvuzisha kwenda mahali fulani kwa wahusika fulani kwa ajili ya "kukata mti na kupanda mti" vijana wa kijiweni wanaita "Kujiachia"

Mwalimu,hapo juu nimekuuliza hivi kweli tunajua kiini cha kuanzishwa kwa siku hiyo na madhumuni yake?Mimi sijui ila bado najaribu kutafuta ukweli katika hilo.Inawezekana waratibu wake hapa nchini(CWT) wanajua.Katika ujumbe wangu huu kwako leo sitaki kabisa kugusia kuhusu CWT na Mustakabali wa taaluma ya Ualimu na Elimu Tanzania kwani ni mada nitakayoizungumzia siku nyingine kipekee.Ila ombi langu kwako ni mabadiliko ya "kimtazamo kuhusu siku ya mwalimu."

Mwalimu! nazungumzia kubadili mtazamo kutoka katika kuadhimisha kwa kufanya mambo tuliyoyazoea na kuangalia namna tunavyoweza kufanya-Professionalization of Teaching profession kwa kutumia siku hii ya mwalimu.Hili linawezekana ikiwa tu walimu wataandaliwa na kupewa nafasi ya kuandika papers na kuziwasilisha katika maadhimisho hayo katika ngazi zote.Yaani kuanzia katika vituo vyao vya kazi hadi kitaifa.Teana ikiwezekana hapa kwetu tuwe na wiki ya mwalimu badala ya siku ya mwalimu.Kwa mwaka huu unaweza kuwa umechelewa kwa kuwa zimebaki siku tatu tu kama sijakosea.Lakini ni matumaini yangu kuwa hii ni nafasi yako kujadili na mwalimu mwenzako na kufikisha ujumbe huu kwa walimu wengine na kuona ni kwa namna gani tunaweza kuifanya siku hii ya mwalimu kuwa ni yenye manufaa zaidi kwa taaluma ya Ualimu na maendeleo ya Elimu nchini.

Mwenzenu,

____________ _________ _________ _________ _________ _________ _
Without "Ethical Culture" there is No Salvation for Humanity
____________ _________ _________ _________ _______