Wednesday, May 27, 2009

JINSI YA KU-BLOCK EMAIL USIZOZITAKA

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikipata malalamiko ya watu kuhusu email address zao kuchukuliwa na watu wasio wajua pasipo ridhaa yao na kuingizwa katika mailing list zao na kuanza kutumiwa email wasizo zihitaji/zisizo wasaidia na kuishia kujaza mailing box zao bila sababu.

Ikiwa hali hiyo imekukuta usiogope kwani ni rahisi sana kuwadhibiti watu hao.Maelezo yafuatayo yatakuwezesha kuondokana na adha za watu hao.

1. Ikiwa upo sehemu ya kusoma/kuandika email, kulia kwa screen yako kuna mahali pameandikwa OPTION. Click hapo.
2. Cahgua mail Option kicha click.
3. Ukurasa utakao funguka kushoto kwako utakuta option kama kumi na mbili hivi.Option ya tatu
iliyoandikwa SPAM.
4. Ukurasa utakaofunguka kulia kwako utakuta option nne.Option ya Pili itakutaka U-Block email.
Fuata maelekezo kwa ku-add email ya mtu usiyetaka akutumie email.
5. Katika ukurasa huo juu ya neno SPAM kuna alama ya
Kompyuta [Save changes] CLICK hapo.
6. Hadi hapo tayari utakuwa umesha ondokana na usumbufu wa kutumiwa email usizohitaji. Kurudi ukurasa mkuu Click neno "mail" lilio juu ya neno YAHOO!MAIL upande wako wa kushoto juu.

Ukifanikiwa mjulishe na mwenzako. Asanye sana na karibu tena katika ukurasa huu.