Saturday, March 27, 2010

HUJUI SIKU YA KUFA.



Kifo kingekuwa kama, kinatoa taarifa.
Kingekuwa kinasema, kesho ni siku ya kufa
Ni wengi wangeungama tusinge jenga gorofa
Hujui siku ya ufa.

Kingesema jiandae, saa kumi ninafariki,
Ujijue baadae, utakwenda kwa Mariki,
Hivyo vizuri ukae, ugawe kile na hiki,
Hujui siku ya kufa.

Kifo kingekuambia, una kufa muda gani,
Tusinge jenga na pia, tusinge kwenda kazini,
Wote tungesubiria, ufe wende kaburini,
Hujui siku ya kufa.

Ni siku ungeijua, una kufa Jumapili,
Gari tusingenunua, tungeuza zote mali,
Kutwa tungeomba dua, tungefanya ya halali,
Hujui siku ya kufa.

Kifo kitu cha pekee, wanyama na Binadamu,
Wadogo hadi wazee, shangazi hadi binamu,
Kifo usikichezee, kina kuhamisha humu,
Hujui siku ya kufa.



 (YOB)

No comments: