Awali ya yote namshukuru Muumba kwa kutuwezesha kuifikia siku ya leo ambapo saa chache zijazo tutauanza mwaka mpya wa 2010.Aidha napenda pia kuchukua nafsi hii kuwashukuru wasomaji wa makala zangu hasa wale wanaoperuzi gazeti langu tando la www.pengotz. blogspot. com.
Pamoja na ukweli kuwa kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikichangia makala katika majukwaa mbalimbali kuhusu walimu na CWT,leo nimeamua kufunga mwaka na makala nyingine kuhusu CWT.Kifupi naweza kusema kuwa makala hii ni mjumuisho wa makala na michango yangu iliyotangulia kuhusu CWT.
CWT ni trade union ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuw walimu hapa nchini wanapata stahili zao kwa wakati.Pamoja na ukweli kuwa CWT imejitahidi kwa kiasi kikubwa sana katika kutekeleza wajibu huo bado chama hicho kina mapungufu kadhaa ya kimuundo na kiutendaji.
Katika makala hii ya kuhitimisha mwaka ningependa kujadili kuhusu swala la uanachama na makato ya ada ya uanachama kama ambavyo nimekuwa nikifanya hapo nyuma.
Kuhusu swala Uanachama,katiba ya CWT inasema kuwa kuna aina tatu za wanachama wa chama hicho.Aina ya kwanza ni wanachama wa heshima ambao hupewa uanachama kutokana na mchango wao kwa chama,Aina ya pili ni uanachama wa hiari na ile ya mwisho ni wanachama wa halisi ambao wanatoa ada ya uanachama kila mwezi.Upungufu uliopo katika kipengele cha wanachama ni katiba kutotoa maelezo ya kutosha kuonyesha namna ya upatikanaji wa hao wanachama halisi.
Jambo jingine ninaloliona kuwa ni upungufu/udhaifu ni kuhusu ada ya uanachama.Tangu nimeifahamu CWT haijawahi kuwa na kiwango sawa cha makato ya ada ya uanachama kwa wanachama wake.CWT imekuwa ikikata 2% ya mshahara wa kila mwalimu kila mwezi kama ada ya uanachama.
Kwa maswala hayo mawili ya uanachama na makato ya ada kwa asilimia 2% ya mshahara wa mwalimu kila mwezi kwangu naliona kuwa ni tatizo kubwa ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka kadri inavyowezekana.
Wakongwe katika sekta ya elimu wanashuhudia kuwa enzi zao walikuwa wakijaza fomu maalumu kwa ajili ya kujiunga na CWT na kila mmoja alipewa nambari ya uanachama pamoja na kadi ya chama.Jambo la kusikitisha hali hiyo siku hizi haipo kwani kila anayeitwa mwalimu na kufundisha shule au chuo cha serikali basi mara moja anaanza kukatwa ada ya uanachama katika mshahara wake pasipo ridhaa yake huku wale walio katika sekta binafsi wakiwekwa kando.!
Aidha, swala la makato ya ada ya uanachama kwa asilimia ya mshahara wa mtu ni aina nyingine ya ufedhuli usioweza kuvumulika wanaofanyiwa walimu hapa nchini.CWT inavuna mamilioni ya pesa za walimu isivyo halali kila mwezi kwa mtindo huo na kutufanya tujiulize hivi CWT-kwa-maslahi- ya-nani?walimu, serikali, AU Viongozi wake?
Nathubutu kusema kuwa CWT inavuna pesa za walimu isivyohalali kila mwezi kutokana na ukweli kuwa kwa mujibu wa sheria zilizopo hawana mamlaka ya kuchukua ada ya uanachama kwa asilimia ya mshahara wa mtumishi.Nasema hayo kwa kuwa nimelazimika katika kuutafuta ukweli kudurusu sheria mabalimbali tangu ile ya mwaka 1961,"The organisation of Tanzania Trade Union Act,1961,[Act no. 20/91],the trade Union(Revocation of special powers) Act,1962,The Trade Union ordiance Act,1962,"The Trade Unions and Trade Disputes (Miscellaneous Provision)Act, 1964 [Act No. 64/64] hadi hii ya sasa iliyofanyiwa marekebisho 2006 "The Trade Union Act,1998 sijaona mahali ambapo wamepewa mamlaka ya aina hiyo isipokuwa kwa sheria ya "Employment and Labour Relations Act,2004 part 4 ndiyo inayotoa maelekezo ya kitu gani kifanyike baada ya mwajiriwa kuridhia mbele ya mashahidi kuhusu makato husika [Sio kwa %] ya mshahara wake kwenda katika trade union husika.
Kwa mantiki hiyo,CWT imekuwa ikuvuna zaidi ya Tshs.3,550,092,000.00/=i kila mwaka tangu mwaka 2002 hadi sasa kutoka kwa walimu pasipo ridhaa yao.Hesabu hiyo hapo juu ni ndogo sana nayo inatokana na walimu waliopatikana kutokana na utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya sekta ya Elimu chini ya programu mbili za MMEM [2002-2006] Ambao uliiwezesha serikali kuajiri walimu wapya 45,796 wa shule za msingi wakati kupitia SEDP [2004-2009] walimu 38,730 wa ngazi ya shahada na stashahada wameajiliwa na kufanya jumla ya walimu wapya walioajiriwa katika sekta ya elimu kati ya mwaka 2002 na 2009 kufikia 84,526.Walimu hao wote hawajawahi kujaza fomu za kujiunga na chama wala kuridhia makato ya ada ya uanachama wa 2% ya mshahara wao.
Ikiwa walimu hao kila mmoja atakuwa anakatwa wastani wa Tshs.3500/- kila mwezi,kwa mwaka mmoja CWT inavuna isivyohalali Tshs. 3,550,092,000. 00/=
Nawaandikia makala hii walimu kwa kuwa naamini kuwa walimu ni watu waelewa,wenye hekima na wanaoamini katika kile wanachokiamini kuwa ni sahihi.Nao watatumia busara zao katika kulitathimini jambo hili na kulitafutia ufumbuzi.
Aidha ,nawaandikia watanzania kwa kuwa naamini kuwa wao ni watu makini,wachambuzi na wenye busara ambao siku zote hawapo tayari kuona uonevu ukifanywa katika jamii yao.Nao watakuwa tayari kuwaunga mkono watu hawa waliopewa jukumu kubwa la malezi ya watoto wetu katika mazingira magumu huku wakinyimwa haki zao za msingi za kiutumishi.
Ninamwandikia katibu mkuu -Hazina na waajiri wote wa walimu [Katibu mkuu,Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi na Wakurugenzi wa halimashauri zote za wilaya] ili watambue kuwa makato wanayoyafanya ya 2% ya mshahara wa kila mwalimu kama ada ya uanachama kwenda CWT sio halali na wanapaswa kusitisha na kuchukua hatua haraka iwezekanavyo.
CWT nao wanapaswa kujipeleleza na kuunda chama imara upya ambacho sio tu kitakuwa kikisimamia na kuratibu upatikanaji wa haki na maslahi ya walimu bali kuhakikisha kuwa kinasimamia ipasavyo maendeleo ya Taaluma ya Ualimu hapa nchini.
Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania.
Nawatakia Kila lakheri katika mwaka Mpya wa 2010.
10 comments:
Huu ni aina ya ufisadi kwa kuwa hatujui kiasi hicho kinapoteaje na hata hatujaona faida au matunda ya chama hiki.
Labda tu kwa ushauri kwa chama hiki, wafungue BANK YA MWALIMU ambayo itakuwa ikiboresha maisha ya mwalimu kwa masharti nafuu kwa kuwa tumeshachangia vya kutosha.
Pia bank hiyo iwe inatoa mikopo rahisi kwa mwalimu ili kuboresha maisha ya mwalimu.
Mfano wa mikopo hiyo ni km vile mwalimu anapotaka kusoma, kujenga nyumba, kununua usafiri nk. badala ya kwenda kwenye makampuni ya kukopesha yanayodunisha maisha ya mwalimu.
Na pia wasitulazimishe waalimu kuwa wanachama wao.
Ila waboreshe huduma km vile kuweka BANK YA MWALIMU itawavutia zaidi waalimu kujiunga wasikae tu wanasubiri migomo eti ndio waseme wanafanya kazi.
Nakiasa chama hiki cha waalimu kuwa wakati wa ndio mzee!!! umepitwa na wakati, na taaluma ya ualimu imevamiwa na wasomi wanaoelewa. Hivyo sasa wawe makini.
JE CHAMA HIKI KWA NINI KISIWE MSTARI WA MBELE KUBORESHA MAISHA YA MWALIMU KWA KUWA NI CHAMA KINACHOONGOZA KWA UTAJIRI.
WALAU KIONESHE MFANO HATA KWA KUANZA NA BAADHI YA NYUMBA ZA WAALIMU.JAMANI WAALIMU HUKO VIJIJINI WANAPATA SANA SHIDA YA NYUMBA. KWA NINI PESA HIZO ZISIFANYE KAZI HIYO? AU MPAKA ISUBIRI PESA YA WAZAZI NA SERIKALI?
Nina mengi sana, lakini walau hayo tu kwa leo.
asante kwa salamu hizi za mwaka mpya Malata.
WAALIMU AMKENI SASA, KUMEKUCHA.
Allan Allen Kaitila,
Thank you Malata for the hot Topics and discussions concerning our teaching professional and teachers status in general.So what should we do then? I always get confused on matters concerning teachers.
Nadhani maoni yako Germinus ya CWT kuwa na account ni wazo zuri.Itakuwa ni vema jamani ili waweze kumkata mwalimu muhusika kwa kipindi maalum. Na siyo kuendelea kutukatakata ovyo, mtu unakatwa CWT weee mpaka basi jamani inauma sana. Mishahara yenyewe bado tunalia haitutoshi,alafu hapo hapo bado tena hako hako kadogo kanachukuliwa jamani tutafika kweli? inauma sana!!!
"Happy New Year 2010"
Sarah C. Edmund (mama Brian)
MA Education
North East Normal University
Renmin Street No 5268
Changchun City,Jilin Province
CHINA
mobile:+86 13134460118
Ahsante malata. I know you use energy in writing these conscious matters pertinent to our profession. Thanks for the attachments you have send. Naomba walimu someni hiyo habari. Inafungua sana akili zetu. Kama kila mwezi CWT inawakata walimu mshahara kwa nini basi isifunguliwe Bank ili mwalimu mwanachama akatwe kwa kipindi maalum halafu baadaye asikatwe tena kwa kuwa hela atayokuwa kakatwa itakuwa iko kwenye mzunguko tayari.
Mimi nilikataa kukatwa na nilimwambia mwajiri kuwa suala la kujiunga CWT ni la hiari lakini mshahara ni haki yangu ya msingi.
Let me tell you one thing, ndio hizi hela mtu anajiandaa kweda kugombea ubunge baada kufanya kazi CWT.
Masikio yetu yasimame.
Germinus Paul Nyeho
Aga Khan University
Tanzania Institute of Higher Education
Institute of Educational Development - Eastern Africa
Salama House, Urambo Street
Mob: +255 747 158 330/ 786 158 330/ 767 148 333
Fax: +255 (0) 22 201 503 75
P. O. Box 125
Dar es Salaam
unajua nini! kwanza inatakiwa tuibane hata kama ni kutukopesha iwe inatukopesha kwa awamu. manake.
Yusufu Ntambala
Ndugu Ntamba na educators wengine,
Naweza nisiwe na jibu la moja kwa moja kuhusu swali lako.Kuna vuguvugu linaendelea mahali fulani.Sipendi kulizungumzia sana hapa sasa.Ila kwa taarifa swala hili linafanyiwa kazi kwa kupitia sheria zilizopo na kuona nani wa kumpeleka hasa kwa pilato,chama, mwajili anaekata pesa yako bila ridhaa yako au wote.Sijajua jamaa wamefikia wapi,labda ni vile nami shule inanikamata kidogo siku hizi.Mambo yakiwa tayari tutapeana taarifa hapa hapa jukwaani.
Samahani kaka, naomba kuuliza, bila shaka swali langu wanaweza kunufaika wengi, "Hivi, kuna uwezekano wa chama cha walimu kumrudishia mwalimu pesa zake ambazo zinakatwa mara tu anapoajiliwa hata kama hajajaza form ya uanachama?"
Kama ulivyoeleza kwenye mail yako, embu tutoe changa la macho, kwa kuwa CWT wanakata pesa kabla ya hata kujaza form zao za uanachama kisheria wakipelekwa kwa pilato inaweza ku-sound? manake wameshakata nyingi sana. embu tafuta tafuta majibu tuone inakuwaje.
Kila la kheri.
Ntambala
Chama cha Walimu ni Wapiga Debe kwa waajiri walimu, Hawana ubavu wa kusaidia mwalimu yeyote nchini. Jaribu kuchunguza mishahara ya walimu na mishahara yao wenyewe, utagundua tayari wamejitenga kwa kujipangia mishahara minono na marupurupu kibao. Lakini tujiulize, tulitarajia Mpiga Debe amsaidie tajiri yupi kati ya hawa :dereva, konda na tajiri. Walimu wana mkataba na mwajiri sio chama cha Walimu. Mpiga Debe ana kiburi kwa sababu ana mahusiano mazuri na tajiri, hili ni tatizo. Mwajiri hawezi kuwa na mahusiano mazuri na mtumishi, na mahusiano yakiboreshwa Mpiga Debe hana chake. Walimu kulazimishwa kukatwa fedha zisaidie chama cha walimu(Mpiga Debe) ni unyonyaji. Kwani wanaopandisha madaraja na TSD, anayelipa mafao ni mwajiri. Kwa nini mwanachama asichangie chama chake kwa hiari badala ya kumlazimisha?
Anyway, I'm sorry for that, "Teachers' problem can be solved by teachers themselves". Teaching can be done by anybody regardless of training, disability which are invisible qualities in other professions. We need to revise this service in our society so that we value education as investment having future returns.
Chama Cha Walimu kuendelea kukata mshahara ya walimu hata kama mtu sio mwanachama ni kuwasaidia wao sio walimu. Walimu watapata unafuu kama waaajiri wao watalipa haki za walimu kadri ya madai yao na si kwa kusikia kelele za CWT. Kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji.
Jamhuri Kidumu
Teacher Educator
Chama cha walimu hakisaidii chochote zaidi ya kutuongezea umasikini kwa kuongeza kiwango cha makato,chama cha walimu hakitusaidii kwa sababu zifuatazo
1. hakina nguvu katika kufuatilia matatizo ya walimu kimetawaliwa na siasa zaidi kuliko utekelezaji hakiwezi hata kugomea mapunjo ya mshaharaka kwa walimu wake, vilevile kinashindwa hata kuchangia uboreshaji wa mazingira ya kazi ya walimu wake mfano mwalimu anatembea umbali mrefu kufuatilia mshahara wake unakuta mwalimu anatumia nusu ya mshahara wake
2. Viongozi wa chama wanachowaza ni kuandikiana malipo ya night kwa ajili ya vikao visivyokua na utekelezaji viongozi wa chama wanajisahau kama nao ni walimu wanasahau kudai haki za walimu
3. CWT hawakumbuki kuongea na walimu wnchokumbuka ni kukata asilimia fulani kutoka kwenye mishahara ya walimu
P. Mushi.
Teacher Educator
Duh! Huu ni wizi/ujambazi bila silaha kama ilivo kwa michango ya harusi!
Wadau nimesoma comments zenu kwa makini sana,this is part of my interest. Nimekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti ngazi ya wilaya kwa kipindi kimoja, mwaka huu pia nagombea.
Chama kina mapungufu ya msingi ikiwemo uwazi katika mapato na matumizi ya fedha. Naomba yeyote mwenye data za wanapata kiasi gani katika makusanyo ya kodi za wapangaji kwenye majengo ya chama anihusishe. Kuna usiri wa hali ya juu! mfumo unaotumika kuwapata watumishi wa chama ni siri tupu! kwa kutaja baadhi.
Kumekuwa na ubaguzi wa chini chini kati ya wakimu wa sekondari na msingi, mfano nilikuwa mgombea pekee wagombea wenzangu walishawishi walimu wa msingi kutokubali nafasi hio kwenda sekondari bila sababu za msingi. Hivyo walitumia wingi wao isivyo halali kupata viongozi. Inasikitisha sana! baadhi ya walimu hawana imani na chama baadhi wanafikiria zaidi kuhama kada baadhi wamekatishwa tamaa baadhi wamekata tamaa wenyewe wengine hawajui la kufanya! binafsi naamini katika mabadiliko sababu mabadiliko ndio maisha. Nyakati siku miaka ngozi na nk hubadilika, so we have to adopt or influence changes but we have to bare the cost! Siamini katika kukata tamaa wala kujidharau sababu hatuna sababu za kujidharau wala kudharaulika. Nimefanya utafiti tofauti za muundo wa mishahara kati ya TGTS na TGS hakuna tofauti! mazingira ya kazi ndio tofauti kubwa. WALIMU WANAPASWA KUBADILI MINDSET! na kuwa na viongozi makini wenye kudhamiria mabadiliko na sio ukomredi tu!
nafatilia nipeni point!
ezra manjerenga.
Post a Comment