Kifo
kingekuwa kama, kinatoa taarifa.
Kingekuwa
kinasema, kesho ni siku ya kufa
Ni
wengi wangeungama tusinge jenga gorofa
Hujui
siku ya ufa.
Kingesema
jiandae, saa kumi ninafariki,
Ujijue
baadae, utakwenda kwa Mariki,
Hivyo
vizuri ukae, ugawe kile na hiki,
Hujui
siku ya kufa.
Kifo
kingekuambia, una kufa muda gani,
Tusinge
jenga na pia, tusinge kwenda kazini,
Wote
tungesubiria, ufe wende kaburini,
Hujui
siku ya kufa.
Ni
siku ungeijua, una kufa Jumapili,
Gari
tusingenunua, tungeuza zote mali,
Kutwa
tungeomba dua, tungefanya ya halali,
Hujui
siku ya kufa.
Kifo
kitu cha pekee, wanyama na Binadamu,
Wadogo
hadi wazee, shangazi hadi binamu,
Kifo
usikichezee, kina kuhamisha humu,
Hujui
siku ya kufa.
(YOB)