Saturday, January 31, 2009

Historia ya South Africa haikamiliki bila mtu huyu.



Historia ya South Africa haiwezi kukamilika bila kumtaja mtu huyu.Na ndio maana huwezi kuingia Chuo kikuu cha Sokoine bila kukutana na Picha hii na maelezo haya katika geti la kuingilia chuoni hapo.Nafikiri tunahitaji kujifunza zaidi kuhusu mtu huyu.Wengi wetu huwa tunapita hapo pasipo hata kujua mtu huyu hasa ni nani na alifanya nini katika kupigania uhuru wa nchi yake.

Thursday, January 22, 2009

Publishers na Mikakati ya kudumaza harakati za waandishi chipukizi.


Zamani zile za ujinga moja ya zoezi kabambe la vyuo vikuu ilikuwa ni kuandika vitabu!?kwa lengo lakukuza moyo wa uandishi kwa vijana wa kitanzania na kuchangia majibu ya kitaalamu kwa maswala mbalimbali katika taifa letu.Waandishi wa vitabu kwa sababu ya kukosa fedha kwa kawaida huwa wanapeleka miswada yao kwamchapishaji [Publisher] ambaye huwa anaaminiwa kuwa na mtaji wa fedha za kutosha kupiga chapa miswada hiyo.Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo malalamiko mengi kutoka kwa wachapishaji na waamdishi kuhusu "Uharamia" katika sekta ya vitabuPamoja na ukweli kuwa uharamia huo unafanywa na watu wanaofahamika lakini hadi sasa hakuna takwimu zinazoonyesha ni kwa kiasi gani tatizo hilo limeshughulikiwa au linashudhulikiwa na vyombo vinavyohusika.

Matokeo ya uharamia huo pamoja na mambo mengine kama urasimu ilipelekea waandishi wengi wenye mitaji[fuko] kidogo kuamua kutowatumia wachapishaji [Publishers] na badala yake kuwatumia wachapaji [Printers] kuchapa vitabu vyao na kuzurura navyo mitaani kutafuta masoko ya vitabu vyao. Sijui ndio ujari wa mali huo!!?

Hali hiyo kwa kiasi kukubwa inachangiwa na sera za makampuni ya uchapishaji ambayo mengi yao yamelekeza nguvu na sehemu kubwa ya mtaji pesa katika uchapaji wa baadhi tu ya aina ya vitabu kama vile vitabu vya kiada ambavyo sokolake lipo wazi zaidi na kuacha aina nyingine za vitabu vikikosa mchapishaji jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wa jamii yetu.

Athari za sera za makampuni hayo ya uchapishaji kwa ubaguzi wa baadhi ya kazi za waandishi hasa waandishi chipukizi hazihitaji elimu ya unajimu kuzibaini.Ni ukweli usiopingika kuwa sera na mipango ya makampuni hayo sio tu zinafifisha moyo wa kupenda kuandika kwa waandishi chipukizi bali pia zinainyima jamii haki ya kupata maarifa [Elimu na ujuzi].Jambo la kusikitisha hakuna anayelisemea hili.Bila shaka ni kutokana na ubinafsi unaojengwa na mfumo wetu dhalimu wa elimu.

Wajibu wetu kama wanazuoni ni kutambua ukweli huu na kufichua mbinu hizi za kizandiki zenye lengo la kufifisha,kudumaza na kuzima kabisa harakati za waandishi chipukizi kushirikisha jamii maarifa[Elimu na ujuzi]: pamoja na kubuni mbinu zitakazo saidia kupunguza au kuondoa kabisa athari hizi.

Wanazuoni tunao wajibu wa kuwa wanafunzi daima,tunapaswa kuchambua bila kukoma sio tu hali ya usomaji wa vitabu hapa nchini bali pia vitabu na aina za vitabu vilivyopo katika muktadha wa utandawazi ili kujifahamisha ni kwa jinsi gani mipango na sera za makampuni ya uchapishaji yanaendeleza ufifishaji na udumizwaji wa uandishi wa vitabu hapa nchini.

Natambua zipo changamoto nyingi sana katika sokola vitabu hasa katika zama hizi za "Ulaji na uteja" [Utandawizi] kama marehemu Profesa Chachage alivyotuzoesha kuita.Lakini changamoto hizo zisiwe kikwazo kwa maendeleo ya taifa letu katika kushirikishana maarifa kupitia vitabu.Kwa kuwa moja ya wajibu wa wanazuoni katika jamii ni kuwa kiungo kati ya utambuzi wa athari na mbadala wa madhila katika jamii,tunapaswa kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu jambo hili.Kwa kufanya hivyo udhati unaweza kujengeka na kutafsiriwa kwa maneno na vitendo vyenye nguvu hali itakayopelekea kuwako na "Nuru katika kiza" sio tu katika sekta ya vitabu bali katika nyanja zingine zote.

Ningependa kumalizia na kuwashauri waandaaji wa tamasha la vitabu la kila mwaka kuwa labda tufikirie kauli mbiu ya tamasha hilo kwa mwaka huu kuwa "Mapambano ya Ukombozi wa Usomaji vitabu katika muktadha wa Utamndawazi" ili kuleta changamoto kwa jamiii na kuikumbusha kuhusu jukumu letu kila mmoja kuhusu ung'amuzi wa elimu na ujuzi unaoweza kupatikana kupitia usomaji wa vitabu.