Tuesday, September 18, 2007

Social Responsibility,Parliament and the Role of Intellectuals

The recent events have created the need for a re-examination of our Society in general and the parliament in particular.While the "Udanganyifu" reporting scandals such as the one which involved Hon.Adam Malima Vs Mengi and Zitto Zuberi Kabwe Vs Hon.Nazir Karamagi and "Ufisadi" katika BoT have been dominating headlines recently,the crisis of confidence resulting from the ongoing scandals is really a symptom of deeper issues that need to be addressed.

What is the deepest issue affecting the survival of the parliamentary system?Clearly, the public perception that criminals,whether of the corruption or else,will not be adequately punished by neither parliament nor justice system.This perception,and the parliamentary decisions that feed it,brings the credibility of the social order into question.

What is the problem with the parliamentary system of Tanzania?This crisis has resulted because the parliamental system is overly focused on traditions such as Itikadi za kichama and what is known as "Umimi" if Not "Ubinafsi".

Samahani I am truly one of the "Swa-english" so be patient when am trying to make clarifications on some concepts.Now, with respect to the subject above,lets examine a bit the recently events.

Matukio ya hivi karibuni yaliyoibuliwa bungeni,particulary hili la kusainiwa kwa mikataba ya madini nje ya nchi na reaction ya baadhi ya wabunge,spika, naibu spika na kukomelewa msumari na karani wa Bunge against mtoa hoja ya msingi(Mh.Zitto) na mwitikio wa jamii kuhusu uamuzi uliochukuliwa na Bunge ni ishara mbaya kwa mwelekeo wa nchi yetu.Imefika wakati sasa,eti Bunge linathubutu kuzuia wawakilishi wa wananchi(Wabunge) na wananchi wenyenye nje ya bunge kujadili mambo yanayowahusu kwa kisingizio cha kuingilia shughuli za Bunge ambalo siku za hivi karibuni limekuwa mithili ya "Kijiwe cha wahuni" kiasi cha kuamua kusigina kanuni zilizowekwa kusimamia shughuli za chombo hicho.
{Rejea kanuni za uendeshaji shughuli za Bunge;kanuni ya 28(1);kanuni ya 44(1);kanuni ya 68(1) na kanuni ya 103(2) against uamuzi uliochukuliwa na chombo hicho dhidi ya Mh.Zitto.}

Wote tunaojua kazi na majukumu ya Bunge tunaelewa wazi kuwa "Kuwanyamazisha wananchi" sio kazi ya Bunge.Ikiwa basi tunaamini kuwa "Msomi" ni yule aliyeenda shule(Formal schooling),basi Bunge letu limesheheni wasomi waliotukuka katika fani mbalimbali.The challenging question remains;What is our role and relevance as Tanzania Intellectuals?

Joseph Mihangwa,mmoja wa waandishi makini wa makala nchini aliwahi kuandika kumwelezea "msomi" kama ifuatavyo;-
"Msomi yeyote anawajibu wa kuelewa na kujihusisha kikamilifu na mambo yote yanayotokea katika jamii yake,na hupimwa uwezo wake kwa jinsi anavyojishirikisha na tabaka la watawala kama yeye si mtawala katika kuleta hali boramkwa jamii yake.

Msomi hapaswi kusubiri kuambiwa afanye nini hali tata inapotokea katika jamii yake.Yeye ni mwepesi wa kutenda na kuleta mabadiliko yanayotakiwa. Ni wajibu wake kuongoza na kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko hayo.Kutofanya hivyo ni uasi kwa jamii unaovuka kiwango cha Uhaini na hivyo hawezi kukwepa kujibu tuhuma za kuiasi jamii yake"
{Wasomi kizimbani,Rai No...,Feb. 27,2003}

Ninapojaribu kutafuta uhusiano wa aina ya watu tulionao ndani na nje ya Bunge,na yale yanayotokea hapa nchini,I come up with the conclusion that "What is missing is an emphasis on social responsibility"

What is meant by social responsibility?Social responsibility involves taking into account the needs of society;the damage to society of the crime;and the impact of any decision on the fabric of that society.The health of the Society is paramount.Note, that does not mean that society can trample on individual rights...that would only negate any social purpose.Rather, it means that individual rights can exist up to the point where society becomes threatened.That does not mean social change cannot occur...since social change is healthy and reflects a vibrancy in that society.Again, it means that society cannot be taken advantage of,in particular for ulterior purposes.

If social responsibility does not become an important consideration in the parliamentary system,them the bleeding of public confidence will continue---and that will serve neither the parliamentary system nor society.Kindly I keep the ball rolling.

Collegially

Pro.Chachage:Msomi wa Jamii ataekumbukwa Daima


Ni mwaka wa tatu  sasa tangu mpendwa wetu Prof. Seithy Chachage alipoiaga dunia. Leo ni siku ya kihistoria kwetu. Ni siku ya kihistoria kwa kuwa tunaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mpendwa wetu, mzazi wetu, mlezi wetu na rafiki yetu. Siku ya leo ni siku inayotuongoza kuyatafakari mambo machache katika maisha yetu yanayoguswa na maisha ya Profesa Chachage (Mungu amlaze mahali pema). Ni siku ya kugeuka na kutazama haiba ya jamii yetu tukizingatia yanayojitokeza katika utashi wa waliotutangulia. Kumbukumbu hii inafanya historia kwetu isiwe mambo ya kale ila mambo yanayotuhusu sasa na kwa matarajio mema ya siku zijazo.

Kwa hiyo basi, historia kwetu iwe ni sasa ikivuviwa na zamani; iwe ni matendo ya sasa yakitiwa nguvu na yale ya waliotutangulia Tunapofanya tafakuri ya maisha ya marehemu Profesa Chachage, ni vema tukaungana na wanafalsafa waliojaribu kuiona historia kama tendo la mtu anayekimbia, akienda mbele anakotaka bila kupafahamu, ila akitazama nyuma kwa tahadhari ya yaliyoishakumgusa.

Kumbukumbu ya leo inatusukuma kuifikia hali ya ukingoni ambayo wanatheolojia wanaiita “ apocalyptic moment”. Hali inayodai ufunuo mpya. Hali tata inayodhihirisha fumbo la maisha yetu . Fumbo hili ni kwamba, kuna pengo kubwa kati ya ukweli wa maisha yetu na jitihada za mantiki tunayotumia ili kuona ukweli huo . Ndio maana tunasimama na kutafakari ;tunatazama maisha ya waliotutangulia ili kupata nguvu za utashi wa sasa unaokidhi haja za kisasa. Tunatafakari maisha ya Profesa Chachage ili tuweze kuyaona maisha yetu vizuri zaidi .Ni kipindi cha kutafakari!

Ujasiri wetu wa kutafakari maisha ya Profesa Chachage huenda ukafananishwa na ule wa Susi na Chuma waliotafakari maisha ya Dr. David Livingstone na kuubeba mwili wake toka Ujiji – Kigoma hadi Bagamoyo akazikwe makwao. Sisi tunatafakari maisha ya mtu aliyeishi pamoja nasi , aliyefanya kazi pamoja nasi. Tunamkumbuka Profesa Chachage kwa mshikamano aliokuwa nao kwetu hadi kufikia mauti yake.

Pamoja na ukweli kuwa ni mwaka mmoja tu tangu alipotutoka,mengi yanayotuzunguka huibua kumbukumbu kumhusu Profesa Chachage. Wengine tumeishi naye ; wengine tumefanya kazi pamoja nae na wengine tumemsikia tu na kuona kazi zake. Hayo yote hudhihirisha azma aliyokuwa nayo katika maisha yake aliyoishi kama “Msomi wa Jamii (Public Intellectual)”

Ninaporejea hotuba kali yenye simanzi ya William Shakespare katika tamthilia ya Julius Kaisari inaonyesha ujasiri wa Marko Antoni katika kumzika Kaisari “…….. maovu watendayo watu hudumishwa baada ya uhai wao , ila mema huzikwa pamoja na mifupa yao…………” Na iwe hivyo kwa Kaisari!”Marko Antoni alisema hayo kwa kuwashutumu mahasimu na Waroma kwa kusahau mema mengi ambayo Kaisari aliwatendea. Nasi leo tunajaribu kuyataja walau machache katika mema mengi ya Profesa Chachage.

Kwa hakika yapo mambo mengi sana mema aliyoyafanya Profesa Chachage katika siku za uhai wake. Profesa Chachage katika uhai wake alijitahidi sana kuitazama haiba ya jamii yetu kwa kuzingatia mambo yanayojitokeza katika utashi wa matendo yetu ili kuleta ufunuo mpya na matarajio mema ya jamii yetu kwa siku za usoni.

Profesa Chachage aliitambua fika “ajali” yetu; ambayo ni kuishi katika bara lililojaa mazonge na madhila, na mzigo wa umaskini. Siku zote alikuwa ni mfuasi mzuri wa dini ya “Ubinadamu” akijitahidi kuikarabati jamii na kupanda mbegu ya ujasiri ili tuweze kuikana mifumo dhalimu inayowalaza watu njaa. Aliamini kuwa tunahitaji uhuru wa fikra na juhudi zetu wenyewe katika kujiletea maendeleo .

Siku zote alikinzana na wasomi wetu ambao wengi wao wamenaswa katika mikoba ya uchawi wa Giningi na kusahau kabisa uganga (Udaktari) ambao wameusomea na kufuzu kwa viwango vilivyotukuka. Alipinga wazi wazi matendo yaliyopanua mpasuko katika jamii baina ya watawala wakwasi wa kupindukia na wananchi maskini hohehahe waishio katikati ya utajiri wa asili.

Kutokana na hulka aliyokuwa nayo ,sio tu aliwaogofya watawala “waliokeneguka” bali pia asasi za kimataifa kila alipokuwa akitoa mwito wa kujali masuala yahusuyo ujenzi wa jamii bora yenye kuzingatia haki , usawa wa binadamu, uhuru , ubinadamu na ukomavu wa kiuchumi. Pamoja na ukweli kuwa juhudi za kujikomboa katika nyanja zote za kujenga Dunia mpya iliyo bora. Mapambano ya kuleta Dunia mbadala ambayo haina ubaguzi, ukandamizwaji, unyonyaji wala ufisadi ina historia ndefu , tangu enzi za mababu zetu. Inasikitisha kuona kuwa kila kukicha wajanja wanakuja na mifumo mipya ya maisha inayotutaka turudi nyuma katika mapambano haya ya kihistoria.

Profesa Chachage hakuna alichopoteza duniani. Alifanya mambo mengi makubwa kwa ajili ya nchi yetu na kuweka “muhuri” wake katika mioyo ya Watanzania. Kama ilivyo kwa shujaa wa “Mapinduzi” Che Guevara , Profesa Chachage tutaendelea kumkumbuka kwa ushujaa wake. Ushujaa wa kuchukua uamuzi mzito kwa ajili ya watu na si wakubwa fulani. Maombolezo ya kifo chake na umati wa watu waliohudhuria mazishi yake ni ushuhuda wa haya yanayosemwa juu ya Profesa Chachage.

Kwa haraka haraka, anayesikiliza tafakuri hii ya maisha ya Profesa Chachage anaweza kusema kuwa inamhusu mtu mmoja mdogo na mahala fulani padogo (Mtwango au Changanyikeni)! Ikumbukwe kuwa wengi tumepita mikononi mwake na kusambaa katika jamii pana. Kwa njia hii maisha ya mtu mmoja yanaweza kuwagusa wengi hata wale ambao hawakukutana nae. Kutafakari kwetu kutukumbushe mbegu ya haradali.
Ni mbegu ndogo sana, ila hupandwa na kuchipua . Inastawi na kuwa mti mkubwa ambao ndege hutua na kuimba juu yake. Mbegu moja huzaa maelfu na kutokana nayo hupatikana msitu mzito.

Kwa hakika leo hatuombolezi. Hatuna majonzi katika kumkumbuka Profesa Chachage . Jambo lililo muhimu kwetu sasa ni kwamba, katika kumkumbuka tunaweza kuchipuka upya kama mbegu ya haradali. Tujifunze kuwa tayari kusimama , kuhoji na kukataa mambo yote yanayotulazimisha kuyakubali yale tusiyoyaafiki .Mambo yanayopingana na itikeli za maisha yetu. Kumbukumbu ya Profesa Chachage inatukumbusha kuepuka kujiuliza, “Nitapata nini nikitenda mema? Hiki ni kipindi kinachohitaji ufunuo mpya!

“Mungu amlaze mahali pema peponi Profesa Chachage”

Adios Amigo

Profesa Seithy Loth Chachage “Mwamwani”